5Njooni, enyi nyumba ya Yakobo, tutembeeni katika nuru ya Bwana.
6Umewatelekeza watu wako, nyumba ya Yakobo. Wamejaa ushirikina utokao Mashariki, wanapiga ramli kama Wafilisti na wanashikana mikono na wapagani.
7Nchi yao imejaa fedha na dhahabu, hakuna mwisho wa hazina zao. Nchi yao imejaa farasi, hakuna mwisho wa magari yao.
8Nchi yao imejaa sanamu, wanasujudia kazi za mikono yao, vitu vile vidole vyao vimevitengeneza.
9Kwa hiyo mwanadamu atashushwa na binadamu atanyenyekezwa: usiwasamehe.