11Hakika anawatambua watu wadanganyifu; naye aonapo uovu, je, haangalii?
12Mpumbavu aweza kuwa mwenye hekima, endapo mtoto wa punda-mwitu atazaliwa mwanadamu.
13“Hata sasa ukiutoa moyo wako kwake na kumwinulia mikono yako,
14ukiiondolea mbali ile dhambi iliyo mkononi mwako wala usiuruhusu uovu ukae hemani mwako,
15ndipo utainua uso wako bila aibu; utasimama imara bila hofu.