6Nitadumisha haki yangu wala sitaiacha; dhamiri yangu haitanisuta muda wote ninaoishi.
7“Watesi wangu wawe kama waovu, nao adui zangu wawe kama wasio haki!
8Kwa maana mtu asiyemcha Mungu analo tegemeo gani anapokatiliwa mbali, Mungu anapouondoa uhai wake?
9Je, Mungu husikiliza kilio chake, shida zimjiapo?
10Je, anaweza kumfurahia Mwenyezi? Je, atamwita Mungu nyakati zote?