8Kwa maana mtu asiyemcha Mungu analo tegemeo gani anapokatiliwa mbali, Mungu anapouondoa uhai wake?
9Je, Mungu husikiliza kilio chake, shida zimjiapo?
10Je, anaweza kumfurahia Mwenyezi? Je, atamwita Mungu nyakati zote?
11“Nitawafundisha juu ya uweza wa Mungu; njia za Mwenyezi sitazificha.
12Ninyi nyote mmeona hili wenyewe. Ni ya nini basi mazungumzo haya yasiyo na maana?