9Je, Mungu husikiliza kilio chake, shida zimjiapo?
10Je, anaweza kumfurahia Mwenyezi? Je, atamwita Mungu nyakati zote?
11“Nitawafundisha juu ya uweza wa Mungu; njia za Mwenyezi sitazificha.
12Ninyi nyote mmeona hili wenyewe. Ni ya nini basi mazungumzo haya yasiyo na maana?
13“Hili ndilo fungu ambalo Mungu humpa mtu mwovu, urithi ule mtu mdhalimu anapokea kutoka kwa Mwenyezi: