13Je, ni nani aliyemtawaza juu ya dunia? Ni nani aliyemweka kuwa mwangalizi wa ulimwengu wote?
14Kama lilikuwa kusudi la Mungu, naye akaiondoa Roho yake na pumzi yake,
15wanadamu wote wangeliangamia kwa pamoja, na mtu angerudi mavumbini.
16“Kama ninyi mnaufahamu, sikieni hili; sikilizeni hili nisemalo.
17Je, yeye aichukiaye haki aweza kutawala? Je, utamhukumu mwenye haki, Aliye na Nguvu Zote?