11yeye atufundishaye sisi zaidi kuliko wanyama wa dunia, na kutufanya wenye hekima kuliko ndege wa angani?’
12Yeye hajibu wakati watu waliapo kwa sababu ya kiburi cha watu waovu.
13Naam, Mungu hasikilizi maombi yao ya ubatili; Mwenyezi hayazingatii.
14Si zaidi sana kwamba hatakusikiliza wewe usemapo humwoni, tena ya kwamba shauri lako liko mbele zake na wewe lazima umngojee,
15pia zaidi, kwamba hasira yake kamwe haiadhibu wala haangalii uovu hata kidogo?