Ayubu 36

Lakini wasiposikiliza, wataangamia kwa upanga, nao watakufa pasipo maarifa.

Job 36:12 (UKJV) But if they obey not, they shall perish by the sword, and they shall die without knowledge.

10Huwafanya wao kusikia maonyo, na huwaagiza kutubu uovu wao.

11Kama wakitii na kumtumikia, wataishi siku zao zilizobaki katika mafanikio, na miaka yao katika utoshelevu.

12Lakini wasiposikiliza, wataangamia kwa upanga, nao watakufa pasipo maarifa.

13“Wasiomcha Mungu moyoni mwao huficha chuki; hata anapowafunga, hawamwombi msaada.

14Wanakufa wangali vijana, miongoni mwa wanaume hanithi wa mahali pa kuabudia miungu.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.