25Wanadamu wote wameiona; watu wanaikazia macho kwa mbali.
26Tazama jinsi Mungu alivyo mkuu, kupita ufahamu wetu! Hesabu ya miaka yake haitafutiki.
27“Yeye huvuta juu matone ya maji, ayachujayo kama mvua kutoka kwenye vijito;
28mawingu huangusha chini maji yake, nayo mvua nyingi huwanyeshea wanadamu.
29Ni nani ajuaye jinsi ayatandazavyo mawingu, jinsi angurumavyo kutoka hemani mwake.