24Kumbuka kuzitukuza kazi zake, ambazo watu wamezisifu katika wimbo.
25Wanadamu wote wameiona; watu wanaikazia macho kwa mbali.
26Tazama jinsi Mungu alivyo mkuu, kupita ufahamu wetu! Hesabu ya miaka yake haitafutiki.
27“Yeye huvuta juu matone ya maji, ayachujayo kama mvua kutoka kwenye vijito;
28mawingu huangusha chini maji yake, nayo mvua nyingi huwanyeshea wanadamu.