22“Mungu ametukuzwa katika nguvu zake. Ni nani aliye mwalimu kama yeye?
23Ni nani aliyemwelekeza katika njia zake, au kumwambia, ‘Wewe umetenda yasiyo sawa’?
24Kumbuka kuzitukuza kazi zake, ambazo watu wamezisifu katika wimbo.
25Wanadamu wote wameiona; watu wanaikazia macho kwa mbali.
26Tazama jinsi Mungu alivyo mkuu, kupita ufahamu wetu! Hesabu ya miaka yake haitafutiki.