27“Yeye huvuta juu matone ya maji, ayachujayo kama mvua kutoka kwenye vijito;
28mawingu huangusha chini maji yake, nayo mvua nyingi huwanyeshea wanadamu.
29Ni nani ajuaye jinsi ayatandazavyo mawingu, jinsi angurumavyo kutoka hemani mwake.
30Tazama jinsi anavyotandaza umeme wa radi kumzunguka, naye huvifunika vilindi vya bahari.
31Hivi ndivyo atawalavyo mataifa, na kuwapa chakula kwa wingi.