Ayubu 41

Je, ataendelea kukuomba umhurumie? Atasema nawe maneno ya upole?

Job 41:3 (UKJV) Will he make many supplications unto you? will he speak soft words unto you?

1“Je, waweza kumvua Lewiathani kwa ndoano ya samaki, au kufunga ulimi wake kwa kamba?

2Waweza kupitisha kamba puani mwake, au kutoboa taya lake kwa kulabu?

3Je, ataendelea kukuomba umhurumie? Atasema nawe maneno ya upole?

4Je, atafanya agano nawe ili umtwae awe mtumishi wako maisha yake yote?

5Je, utamfuga na kumfanya rafiki kama ndege, au kumfunga kamba kwa ajili ya wasichana wako?

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.