3Je, ataendelea kukuomba umhurumie? Atasema nawe maneno ya upole?
4Je, atafanya agano nawe ili umtwae awe mtumishi wako maisha yake yote?
5Je, utamfuga na kumfanya rafiki kama ndege, au kumfunga kamba kwa ajili ya wasichana wako?
6Je, wafanyabiashara watabadilishana bidhaa kwa ajili yake? Watamgawanya miongoni mwa wafanyao biashara?
7Je, waweza kuijaza ngozi yake kwa vyuma vyenye ncha kali, au kichwa chake kwa mkuki wa kuvulia samaki?