2“Hata lini wewe utasema mambo kama haya? Maneno yako ni kama upepo mkuu.
3Je, Mungu hupotosha hukumu? Je, Mwenyezi hupotosha kile kilicho haki?
4Watoto wako walipomtenda dhambi, aliwapa adhabu ya dhambi yao.
5Lakini ukimtafuta Mungu, nawe ukamsihi Mwenyezi,
6ikiwa wewe ni safi na mnyofu, hata sasa atainuka mwenyewe kwa niaba yako, na kukurudisha katika mahali pako pa haki.