Nehemia 11

Jumla ya Walawi waliokaa katika mji mtakatifu walikuwa watu 284.

Nehemiah 11:18 (UKJV) All the Levites in the holy city were two hundred fourscore and four.

16Shabethai na Yozabadi, viongozi wawili wa Walawi, ambao walisimamia kazi za nje za nyumba ya Mungu;

17Matania mwana wa Mika, mwana wa Zabdi, mwana wa Asafu, kiongozi aliyeongoza kutoa shukrani na maombi; Bakbukia aliyekuwa msaidizi wake kati ya wenzake; na Abda mwana wa Shamua, mwana wa Galali, mwana wa Yeduthuni.

18Jumla ya Walawi waliokaa katika mji mtakatifu walikuwa watu 284.

19Mabawabu: Akubu, Talmoni na wenzao, waliolinda malango: watu 172.

20Waisraeli waliosalia, pamoja na makuhani na Walawi, walikuwa katika miji yote ya Yuda, kila mmoja katika urithi wa baba yake.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.