16Kwa hiyo Mose akawahesabu, kama alivyoamriwa na neno la Bwana.
17Haya yalikuwa majina ya wana wa Lawi: Gershoni, Kohathi na Merari.
18Haya ndiyo yaliyokuwa majina ya koo za Wagershoni: Libni na Shimei.
19Koo za Wakohathi zilikuwa ni: Amramu, Ishari, Hebroni na Uzieli.
20Koo za Wamerari zilikuwa ni: Mahli na Mushi. Hizi ndizo zilizokuwa koo za Walawi, kufuatana na jamaa zao.