Mithali 23

Usitamani vyakula vyake vitamu kwa kuwa chakula hicho ni cha hila.

Proverbs 23:3 (UKJV) Be not desirous of his dainties: for they are deceitful food.

1Uketipo kula chakula na mtawala, angalia vyema kile kilicho mbele yako,

2na utie kisu kooni mwako kama ukiwa mlafi.

3Usitamani vyakula vyake vitamu kwa kuwa chakula hicho ni cha hila.

4Usijitaabishe ili kuupata utajiri, uwe na hekima kuonyesha kujizuia.

5Kufumba na kufumbua utajiri hutoweka, huwa kama umepata mabawa ghafula, ukaruka na kutoweka angani kama tai.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.