15Kuhusu mwanadamu, siku zake ni kama majani, anachanua kama ua la shambani;
16upepo huvuma juu yake nalo hutoweka, mahali pake hapalikumbuki tena.
17Lakini kutoka milele hata milele upendo wa Bwana uko kwa wale wamchao, nayo haki yake kwa watoto wa watoto wao:
18kwa wale walishikao agano lake na kukumbuka kuyatii mausia yake.
19Bwana ameweka imara kiti chake cha enzi mbinguni, ufalme wake unatawala juu ya vyote.