3akusamehe dhambi zako zote, akuponya magonjwa yako yote,
4aukomboa uhai wako na kaburi, akuvika taji ya upendo na huruma,
5atosheleza mahitaji yako kwa vitu vyema, ili ujana wako uhuishwe kama wa tai.
6Bwana hutenda haki, naye huwapa hukumu ya haki wote wanaoonewa.
7Alijulisha Mose njia zake, na wana wa Israeli matendo yake.