108Ee Bwana, pokea sifa za hiari za kinywa changu, nifundishe sheria zako.
109Ingawa maisha yangu yako hatarini siku zote, sitasahau sheria yako.
110Waovu wamenitegea mtego, lakini sijayakiuka maagizo yako.
111Sheria zako ni urithi wangu milele, naam ni furaha ya moyo wangu.
112Nimekusudia moyoni mwangu kuyafuata maagizo yako mpaka mwisho.