137Ee Bwana, wewe ni mwenye haki, sheria zako ni sahihi.
138Sheria ulizoziweka ni za haki, ni za kuaminika kikamilifu.
139Jitihada yangu imenidhoofisha, kwa kuwa adui zangu wanayapuuza maneno yako.
140Ahadi zako zimejaribiwa kikamilifu, mtumishi wako anazipenda.
141Ingawa ni mdogo na ninadharauliwa, sisahau mausia yako.