152Tangu zamani nimejifunza kutoka shuhuda zako kwamba umezithibitisha ili zidumu milele.
153Yaangalie mateso yangu, uniokoe, kwa kuwa sijasahau sheria yako.
154Nitetee katika hali hii yangu na unikomboe, uyahifadhi maisha yangu sawasawa na ahadi yako.
155Wokovu uko mbali na waovu, kwa kuwa hawatafuti maagizo yako.
156Ee Bwana, huruma zako ni kuu, uyahifadhi maisha yangu sawasawa na sheria zako.