53Nimeshikwa sana na ghadhabu kwa ajili ya waovu, ambao wameacha sheria yako.
54Maagizo yako ni kiini cha nyimbo zangu popote ninapoishi.
55Ee Bwana, wakati wa usiku ninalikumbuka jina lako, nami nitatii sheria yako.
56Hili limekuwa zoezi langu: nami ninayatii mausia yako.
57Ee Bwana, wewe ni fungu langu, nimeahidi kuyatii maneno yako.