54Maagizo yako ni kiini cha nyimbo zangu popote ninapoishi.
55Ee Bwana, wakati wa usiku ninalikumbuka jina lako, nami nitatii sheria yako.
56Hili limekuwa zoezi langu: nami ninayatii mausia yako.
57Ee Bwana, wewe ni fungu langu, nimeahidi kuyatii maneno yako.
58Nimetafuta uso wako kwa moyo wangu wote, nihurumie sawasawa na ahadi yako.