2Unajua ninapoketi na ninapoinuka; unatambua mawazo yangu tokea mbali.
3Unafahamu kutoka kwangu na kulala kwangu; unaelewa njia zangu zote.
4Kabla neno halijafika katika ulimi wangu, wewe walijua kikamilifu, Ee Bwana.
5Umenizunguka nyuma na mbele; umeweka mkono wako juu yangu.
6Maarifa haya ni ya ajabu mno kwangu, ni ya juu sana kwangu kuyafikia.