4Kabla neno halijafika katika ulimi wangu, wewe walijua kikamilifu, Ee Bwana.
5Umenizunguka nyuma na mbele; umeweka mkono wako juu yangu.
6Maarifa haya ni ya ajabu mno kwangu, ni ya juu sana kwangu kuyafikia.
7Niende wapi nijiepushe na Roho yako? Niende wapi niukimbie uso wako?
8Kama nikienda juu mbinguni, wewe uko huko; nikifanya vilindi kuwa kitanda changu, wewe uko huko.