5Upendo wako, Ee Bwana, unafika hadi mbinguni, uaminifu wako hadi kwenye anga.
6Haki yako ni kama milima mikubwa, hukumu zako ni kama kilindi kikuu. Ee Bwana, wewe huwahifadhi mwanadamu na mnyama.
7Upendo wako usiokoma ni wa thamani mno! Watu wakuu na wadogo hujificha uvulini wa mbawa zako.
8Wanajifurahisha katika wingi nyumbani mwako, nawe utawanywesha katika mto wa furaha zako.
9Kuwa pamoja nawe ni kijito cha uzima, katika nuru yako twaona nuru.