7Upendo wako usiokoma ni wa thamani mno! Watu wakuu na wadogo hujificha uvulini wa mbawa zako.
8Wanajifurahisha katika wingi nyumbani mwako, nawe utawanywesha katika mto wa furaha zako.
9Kuwa pamoja nawe ni kijito cha uzima, katika nuru yako twaona nuru.
10Dumisha upendo wako kwa wale wanaokujua wewe, haki yako kwa wale walio wanyofu wa moyo.
11Mguu wa mwenye kiburi usije dhidi yangu, wala mkono wa mwovu usinifukuze.