Zaburi 37

Wenye haki watairithi nchi, na kuishi humo milele.

Psalm 37:29 (UKJV) The righteous shall inherit the land, and dwell therein for ever.

27Acha ubaya na utende wema, nawe utaishi katika nchi milele.

28Kwa kuwa Bwana huwapenda wenye haki naye hatawaacha waaminifu wake. Watalindwa milele, lakini uzao wa waovu utakatiliwa mbali.

29Wenye haki watairithi nchi, na kuishi humo milele.

30Kinywa cha mwenye haki hutamka hekima, nao ulimi wake huzungumza lililo haki.

31Sheria ya Mungu wake imo moyoni mwake; nyayo zake hazitelezi.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.