29Wenye haki watairithi nchi, na kuishi humo milele.
30Kinywa cha mwenye haki hutamka hekima, nao ulimi wake huzungumza lililo haki.
31Sheria ya Mungu wake imo moyoni mwake; nyayo zake hazitelezi.
32Watu waovu huvizia wenye haki, wakitafuta kuwaua;
33lakini Bwana hatawaacha mikononi mwao wala hatawaacha wahukumiwe kuwa wakosa wanaposhtakiwa.