1Ee Mungu, ufanye haraka kuniokoa; Ee Bwana, njoo hima unisaidie.
2Wale wanaotafuta kuuondoa uhai wangu, waaibishwe na kufadhaishwa; wote wanaotamani kuangamizwa kwangu, warudishwe nyuma kwa aibu.
3Wale waniambiao, “Aha! Aha!” warudi nyuma kwa sababu ya aibu yao.