7Katika shida yako uliniita nami nikakuokoa, nilikujibu katika mawingu yenye ngurumo; nilikujaribu katika maji ya Meriba.
8“Enyi watu wangu, sikieni, nami nitawaonya: laiti kama mngenisikiliza, ee Israeli!
9Hamtakuwa na mungu mgeni miongoni mwenu; msimsujudie mungu wa kigeni.
10Mimi ni Bwana Mungu wako, niliyekutoa nchi ya Misri. Panua sana kinywa chako nami nitakijaza.
11“Lakini watu wangu hawakutaka kunisikiliza; Israeli hakutaka kunitii.