1Ee Bwana, tegea sikio maneno yangu, uangalie kupiga kite kwangu.
2Sikiliza kilio changu ili unisaidie, Mfalme wangu na Mungu wangu, kwa maana kwako ninaomba.
3Asubuhi, unasikia sauti yangu, Ee Bwana; asubuhi naleta haja zangu mbele zako, na kusubiri kwa matumaini.
4Wewe si Mungu unayefurahia uovu, kwako mtu mwovu hataishi.