28Wafutwe kutoka kitabu cha uzima na wasiorodheshwe pamoja na wenye haki.
29Mimi niko katika maumivu na dhiki; Ee Mungu, wokovu wako na unihifadhi.
30Nitalisifu jina la Mungu kwa wimbo, nami nitamtukuza kwa kumtolea shukrani.
31Hili litampendeza Bwana kuliko ngʼombe dume, zaidi ya fahali akiwa na pembe na kwato zake.
32Maskini wataona na kufurahi: ninyi mnaomtafuta Mungu, mioyo yenu na iishi!