16alitoa vijito kutoka kwenye jabali lililochongoka, akayafanya maji yatiririke kama mito.
17Lakini waliendelea kutenda dhambi dhidi yake, wakiasi jangwani dhidi ya Aliye Juu Sana.
18Kwa makusudi walimjaribu Mungu, wakidai vyakula walivyovitamani.
19Walinena dhidi ya Mungu, wakisema, “Je, Mungu aweza kuandaa meza jangwani?
20Alipopiga mwamba, maji yalitoka kwa nguvu, vijito vikatiririka maji mengi. Lakini je, aweza kutupa chakula pia? Je, anaweza kuwapa watu wake nyama?”